Historia ya Tick

Fikia kumbukumbu ya data ya tick kihistoria inayotolewa kutoka kwa bei zetu za wakati halisi. Chagua instrument na muda wa kupakua faili ya zipu ya bei za awali za bid na ask.

Kumbuka: Ili kutazama historia ya tick kwa miezi iliyopita, unahitaji kupakua historia ya mwezi mzima. Unaweza tu kuchagua siku mahususi kwa mwezi wa sasa.

Maswali yanayoulizwa sana

Haya hapa ni maswali yetu yanayoulizwa sana kuhusu historia ya tick ya Exness.

Tick ni kipimo cha mabadiliko ya chini zaidi katika bei ya amana ambayo inaweza kwenda juu au chini. Inaweza pia kurejelea mabadiliko ya bei ya instrument kutoka trade moja hadi nyingine.

Historia ya tick ni orodha ya tick zote za instrument iliyochaguliwa kwa kipindi fulani cha wakati. Historia ya tick ina matumizi kadhaa, ikiwa ni pamoja na, lakini sio tu, kujaribu mkakati wa biashara au kulinganisha bei ya broker mmoja na mwingine.

Uwazi ni mojawapo ya kanuni za msingi tunazotumia kwa kila kitu tunachofanya katika Exness, na historia yetu ya tick inayopatikana hadharani inathibitisha kanuni hii.

Kwa kutumia historia ya tick unaweza kuthibitisha ubora wa bei ya Exness na kupata ashirio la mahali ambapo soko lilikuwa likitrade kwa kipindi fulani cha wakati fulani. Tafadhali kumbuka kuwa historia ya tick iliyotolewa kwenye ukurasa huu ni elekezi na kwa madhumuni ya kutoa taarifa pekee. Ikiwa una maswali kuhusu execution ya orders zako, wasiliana na timu yetu ya usaidizi.

Faili iliyopakuliwa ina tick zote - bei za bid na ask, kwa instrument iliyochaguliwa na kipindi cha kutrade.

Ili kutafuta bei fulani, unaweza kutumia kipengele cha utafutaji kwenye ripoti ya historia ya tick.

Kumbuka: Buy orders hufunga kwa bei ya bid na sell orders hufunga kwa bei ya ask.

Ikiwa unakabiliwa na matatizo ya kufungua ripoti ndefu za kila mwezi kwenye programu yako ya Numbers kwa MacOS au Excel kwa Windows, unaweza kufungua faili iliyopakuliwa kwa kutumia njia zifuatazo:

  • Programu ya TextEdit kwenye MacOS

  • Programu ya Notepad kwenye Windows

Je, uko tayari kuanza?

Inachukua dakika 3 pekee kuweka mipangilio ya akaunti yako na kuwa tayari kufanya biashara